Biasharika Challenge

Benki ya NMB imezindua rasmi challenge kwa ajili ya vijana wajasiriliamali – ‘Biasharika Challenge’. Ni nafasi yako kushinda mtaji kwa ajili ya biashara yako. Tuma idea yako ambayo unategemea itasaidia kukuza au kubadilisha mwenendo wa biashara yako.

Zawadi:

  • Zaidi ya shilingi milioni 10 kushindaniwa
  • Mafunzo ya kibiashara kutoka SIDO
  • Kujiunga na Business Club zetu ukutane na wafanyabiashara wenzako kubadilishana ujuzi, kupata connection n.k.

Vigezo :

  • Uwe Mtanzania mwenye miaka 18 – 35
  • Uwe tayari na biashara
  • Uwe na NMB Fanikiwa au Mkulima akaunti
  • Uwe na kiwango Zaidi ya shilingi 20,000 kwenye akaunti yako.
  • Wazo lako litapimwa kulingana na utendaji na uhalisia wake.
  • Mshiriki atajiweka kwenye nafasi ya kupata points nyingi zaidi akipost kwenye instagram/ facebook neno "Ombi lako limepokelewa" baada ya kuwasilisha ombi lako, follow na kututag @gonanmb na marafiki zako watatu watakaonufaika kwa kujiunga na hii challenge.

Jinsi ya kushiriki:

  • Jaza fomu hapo chini.
  • Upload video ya chini ya dakika 5 na isizidi MB 100 ukielezea vitu vifuatavyo:
    • Unafanya biashara gani na kama biashara yako ipo hai/haipo hai, tuambie kwanini,
    • Idea yako ya kukuza au kubadilisha mwenendo wa biashara yako,
    • Challenge kubwa unayoipata kwenye biashara yako,
    • Mtaji kutoka NMB utakusaidiaje na hio challenge yako,
    • Tuambie kwanini wewe uwe mshindi.

Similar deals

Card image cap

Expires : Aug 27, 21

View Terms
Mastaboda Loan